Hiki ndicho kiwango alichopendekeza Ay, kulipwa wasanii wakubwa kwa shoo

Malipo ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania katika shows ni sehemu ya kilio cha wasanii hao ingawa wapo wachache wanaotangaza kuneemeka na kipato hicho.

Akiwa katika Maskani ya 100.5 Times Fm na Gardner G Habash, msanii wa kimataifa Ambwene Yesaya amependekeza kuwa wasanii wakubwa wa Tanzania (A-List) walipwe wastani wa shilingi milioni kumi na tano (15,000,000) kwa show moja ili kukuza zaidi kiwanda cha muziki.



AY ameeleza kuwa endapo wasanii wakubwa watalipwa vizuri itakuwa nafasi nzuri ya wao kuongeza nguvu na kufanya show nzuri zaidi ili waongezewe kipato na wasishuke. Lakini pia kiwango hicho kitawahamasisha zaidi wasanii walio katika madaraja mengine ya chini kuongeza bidii ili kufikia kiwango hicho.

Ameongeza kuwa endapo wasanii watakuwa wanalipwa vizuri watatoa ajira zaidi kwa watu wengine wakiwemo dancers, wauzaji wa nguo za shows, watu wa back vocals, wasaidizi binafsi na wengine.

Hivi sasa msanii anaelipwa kiasi kikubwa zaidi kwa shows za ndani ni Diamond Platinumz. Kwa mujibu wa meneja wake, Babu Tale hawafanyi shows nchini bila Tsh. 15,000,000.

Hata hivyo kiwango hiki kina utofauti mkubwa na viwango vya wasanii wengine wakubwa nchini wanaofanya shows za nyumbani.
Previous Post Next Post