Gabrielle Union na Dwyane Wade watua Tanzania kwaajili ya honeymoon

Muigizaji wa filamu wa Marekani, Gabrielle Union na mchezaji wa NBA, Dwyane Wade waliofunga ndoa hivi karibuni, wametua Tanzania kwaajili ya honeymoon.


Mastaa hao waliofunga ndoa Aug. 30, wamekuwa wakishare picha kwenye mtandao wa Instagram zinazonesha bata wanazokula kwenye fungate lao katika maeneo mengi duniani. “When the Indian Ocean is ya swimming pool… You dive in! But first… Play that @beyonce baby,” Union, 41, aliandika kwenye Instagram.

Wakiwa Tanzania, jana wawili hao walitembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti na kupiga picha na wamasai kadhaa.

“Pure joy! Life on the Serengeti… #Tanzania #Masai #2ndLeg … I emoji️ the photographer #BrianFellows,” ameandika Union kwenye picha hiyo.
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA