FBI yachunguza kuvuja kwa picha chafu za mastaa

Shirika la upelelezi la Marekani (FBI) linachunguza tuhuma kwamba picha za siri za watu maarufu ziliibiwa na kutumwa mtandaoni.

Mastaa hao wapatao 20, akiwemo muigizaji wa kike wa Marekani Jennifer Lawrence, naye picha zake zilivujishwa kwenye mtandao wa Internet.


Inafahamika kuwa baadhi ya picha picha hizo zilipatikana katika huduma ya Apple iCloud ambayo husaidi ujumbe uliopo mtandaoni.

Apple nao imesema inachunguza kuwa kama akaunti ya iCloud ilifanyiwa udukuzi.

Bi Lawrence, ambaye ni nyota katika filamu za The Hunger Games, ameomba kufanywa uchunguzi baada ya mdukuzi kupata picha, zenye ujumbe wa picha, kutoka simu za mkononi za mastaa kadhaa.

Msemaji wa FBI aliiambia Associated Press kwamba “wako makini na tuhuma hizo na
wanalishughulikia suala hilo”.

Huduma ya Apple iCloud ndio iliyomsaidia mdukuzi asiyejulikana kuchukua picha chafu za Jennifer Lawrence na mastaa wengine 100 na kuzivujisha mtandaoni.

Naye msemaji wa Apple Nat Kerris alinukuliwa na Reuters akisema kwenye barua pepe; “Huwa tunalinda faragha za watumiaji kwa umakini mkubwa na tunachunguza ripoti hii.”
Previous Post Next Post

Popular Items