Dr Dre ndiye mwana Hip Hop mwenye cash zaidi, awazidi Jay Z na P Didy

Jarida maarufu Duniani la Forbes limetoa orodha yake ya wasanii wa Hip Hop wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani kwa mwaka huu, ‘The 2014 Hip-Hop Cash Kings’ na Dr Dre amekamata nafasi ya kwanza kwa mara nyingine.



Dre Dre amepewa ufalme huo kwa kutengeneza $620 million kupitia biashara zake, na kumfanya arudi kwenye nafasi ya kwanza aliyoikamata mwaka 2012 kabla ya kuenguliwa na Diddy mwaka jana huku yeye akijikuta kwenye nafasi ya tatu.

Pamoja na kwamba Dre hajatoa album wala kufanya tour yoyote kwa miezi 12 iliyopita, lakini dili la Apple kuinunua kampuni yake ya Beats Electronics kwa $3 billion ndio imemfanya atengeneze fedha nyingi zaidi.



Jay Z na P.Diddy wamefungana kwenye nafasi ya pili kwa kutengeneza $60 million kila mmoja.





Drake amekamata nafasi inayofuata kwa kutengeneza $33 million, zilizotokana na album yake ya ‘Nothing Was The Same’, endorsement deal yake na Nike pamoja na tour.

Orodha kamili:

1. Dr. Dre: $620 million
2. Jay Z: $60 million
2. Diddy: $60 million
4. Drake: $33 million
5. Macklemore & Ryan Lewis: $32 million
6. Kanye West: $30 million
7. Birdman: $24 million
8. Lil Wayne: $23 million
9. Pharrell: $22 million
10. Eminem: $18 million
11. Nicki Minaj: $14 million
12. Wiz khalifa: $13 million
13. Pitbull: $12 million
14. Snoop Dogg: $10 million
15. Kendrick Lamar: $9 million
16. Ludacris: $8 million
16. Tech N9ne: $8 million
16. Swizz Beatz: $8 million
16. 50 Cent: $8 million
20. Rick Ross: $7 million
20. J. Cole: $7 million
20. DJ Khaled: $7 million
20. Lil Jon: $7 million
20. Mac Miller: $7 million
Previous Post Next Post