Bow Wow amvisha pete ya uchumba girlfriend wake mtangazaji wa TV

Rapper na mtangazaji wa kipindi cha 106 & Park cha BET, Shad Mos aka Bow Wow amemvisha pete ya uchumba girlfriend wake ambaye ni mtangazaji wa reality show ya Marekani ‘Love & Hip Hop’, Erica Mena.


Bow wow ameshare picha waliyopiga pamoja huku kidole cha mpenzi wake kikiwa kimezungushiwa uzio wa pete ya almasi.




Erica ambaye pia ni muigizaji, amekuwa girlfriend wa Bow wow kwa zaidi ya miezi sita sasa. Ripoti zinadai kuwa uhusiano wao ulizaliwa baada ya Erica kualikwa kwenye kipindi cha 106 & Park ambacho Bow Wow anakiongoza, na siku hiyo wawili hao wali-kiss live kwenye kipindi hicho.

Previous Post Next Post