Baada ya kushambuliwa jijini Paris, sasa Kanye West na Mke wake Kim waajiri walinzi wenye silaha

Kim na Kanye Licha ya kuwashangaza watu wengi kwa nguo zao walizovaa wakati wa Paris Fashion Week, sasa itakuwa ngumu zaidi kuwasogelea au kuwagusa Kanye na mke wake Kim.



Kim Kardashian akisongwa na umati mkubwa wa watu


Kim Kardashian, 33, na Kanye West, 37, wanadaiwa kuwa na wasiwasi mkubwa baada ya kushambuliwa wakiwa red carpet na mwandishi wa habari wa zamani, Vitalii Sediuk kiasi cha kutaka kumwangusha chini Kim.




Wakati mrembo huyo alipokuwa akitoka kwenye gari kwenda kumshuhudia mdogo Kendall Jenner, 18, akishiriki kwenye show hiyo, Vitalii anadaiwa kumvuta nywele Kim huku Kanye na mama yake wakishuhudia.



Kutokana na tukio hilo, Kim na Kanye wamedaiwa kuajiri walinzi wenye silaha za moto watakaokuwa wakimlinda muda wote akiwa Paris.



Wanandoa hao wametengeneza headlines jijini humo kwa aina ya nguo wanazovaa.


Previous Post Next Post