Audio: Sisikii ni kwa ajili ya wote wala sio kwa ajili ya Vanessa Mdee 'Jux'

Msanii wa muziki Jux Vuitton amesema kuwa, kufanya ngoma kama Sisikii ambayo ameandikiwa na staa wa muziki Mabeste, ni moja ya idea ambazo ya tofauti ya mapenzi ambayo haimhusu moja kwa moja na inagusa kwa ujumla maisha ya kimapenzi ya mtu yoyote.

Jux
Music Artist
Jux amesema kuwa anashukuru kuona mapokezi mazuri ya kazi hii ambayo inawalenga moja kwa moja wale wanaopata changamoto ya kupenda mpenzi ambaye haoni umuhimu wa hisia za wenzi wao.



Vilevile Jux akajaribu kueleza ni kwanini anafikiri Jamii inamhusisha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Vanessa Mdee ambapo amedai watanzania ni rahisi sana kujiongeza kuwahusisha watu7 kuwa katika mahusiano pale wanapoona ukaribu wa watu wa jinsia tofauti mara kwa mara, akimaanisha kuwa yeye na Vanessa ni Marafiki tu.


Msikilize Jux hapa akiongea

Previous Post Next Post