Wasanii wa Serengeti Fiesta Tanga wamtembelea Mzee Njenje, azungumzia alivyopatwa na Kiharusi

Msanii mkongwe wa muziki wa dansi Mabrouk Omar a.k.a Babu  Njenje (kushoto), akiongea na wasanii wa muziki wa kizazi kipya walipomtembelea nyumbani kwake mjini Tanga , msanii huyo kwa sasa anasumbuliwa na matatizo ya kiafya.


 Wasanii hao wapo katika msafara wa tamasha ya Serengeti fiesta ambapo kwa mjini hapo linafanyika katika Uwanja wa Mkwakwani.



Mkurugenzi wa  Uzalishaji  na Vipindi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba (kushoto) na Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney wakiteta na  Masanii mkongwe wa muziki wa dansi, Babu Njenje alipotembelewa na timu ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya ili kumpa mkono wa pole.


Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi, Babu Njenje (wa tatu kulia) waliokaa, akipozi kwa picha na baadhi ya wasanii Serengeti fiesta pamoja na baadhi ya watu wengine wenye mapenzi mema walimpomtembelea nyumbani kwake mjini Tanga.


Msanii wa Muziki wa kizazi kipya , Jux akimsalimia msanii mkongwe wa dansi, Babu Njenje wakati wasanii hao walipomtembelea nyumbani kwake mjini Kanga….
Msanii mkongwe wa muziki nchini anayetambulika kwa kazi yake kupitia Kilimanjaro Band, Mzee Njenje anayesumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi ametembelewa na wasanii mbalimbali walioko kwenye Serengeti Fiesta 2014 mjini Tanzania na kuzungumza naye kuhusiana na afya yake pamoja na kupata nasaha zake.
Akizungumza na waandishi leo akiwa nyumbani kwake maeneo ya Sahare Tanga Mzee Njenje amesema anashukuru Mungu kwakuwa sasa hivi anaendelea vizuri japo mwili hauna nguvu.
“Mimi nimepata stroke, sio kali kabisa lakini imeniathiri upande wa kushoto, mguu na mkono, sio mwili wote ni baadhi tu, ni mguu na mkono tu, sehemu ya kichwa iko safi,” amesema. “Hivi juzi nilikwenda nikafanya kukumbuka ya nyimbo zangu nikakumbuka nyimbo zangu kumi, ndio maana nikasema bado nipo strong ni mguu tu unaonisumbua unakuwa na ganzi. ”
“Nimeanza kuumwa tangu tarehe 9 December, tarehe ambayo nilienda kufanya show pale Escape, nilikuja nikaperform nikarudi nyumbani alfajiri nimeamka nikaenda chooni nikasikia mwili hauna nguvu,” ameongeza.

“Lakini nashukuru sikuanguka, nilikaa kwenye kiti cha choo, wakanipeleka hospitali lakini baadaye nivyotoka hospitali wakaja jamaa kunifanyia massage. Hiyo ndio iliyoniumiza walitumia nguvu sana, kwahiyo wakawa wamenirudisha nyuma, lakini nashukuru kuna bimkubwa mmoja ndo ananisaidia sana. Mpaka sasa hivi bado nashindwa kujisaidia mwenyewe ingawa nazungumza vizuri.”

Baada ya kumjulia hali Mzee Njenje, wasanii walielekea kufanya interview katika kituo cha radio cha Breeze FM.
Previous Post Next Post

Popular Items