Video: Keyshia Cole - She

Mwanadada Keyshia Cole - She ameachia video yake mpya inayokwenda kwa jina la SHE wimbo umetayarishwa na DJ Mustard. Katika video hii, muimbaji huyo aliyeachana hivi karibuni na mume wake Daniel “Boobie” Gibson, anaonekana akimchezea kiuchokozi msichana mwenzake chumbani ambaye anaonekana kufanana naye sura.


Hata hivyo Keyshia amedai kuwa wimbo huo hauhusu uhusiano kati ya mwanamke na mwanamke. Wimbo huu utakuwepo kwenye album yake ya sita, ‘Point of No Return’ aliowashirikisha wakali kama Wale, Future, 2 Chainz, na August Alsina, huku akitumia wapishi wa muziki kama Mike WiLL Made-It, Stargate, Mario Winans,na RedOne.
Previous Post Next Post