Video: Fistula Ice Bucket Challenge, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania ajimwagia maji ya barafu kujiunga na kampeni

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Airtel Tanzania, Sunil Colaso amejimwagia maji ya barafu kuashiria kampuni yake kujiunga na kampeni iliyoanzishwa na Vodacom kuchangia matibabu na elimu kuhusu ugonjwa wa Fistula unaowapata akina mama wajawazito zaidi ya 30,000 nchini.

Airtel Tanzania wamepost picha kwenye ukurasa wao wa Instagram na video katika channel yao ya YouTube ikimuonesha mkurugenzi huyo akijimwagia ndoo ya maji kuashiria kukubali challenge baada ya kutajwa na mkurugenzi wa Vodacom, Rene Meza aliyemwagiwa ndoo ya maji Jumatatu.


Rene Meza aliwanominate Mkurugenzi huyo wa Airtel Tanzania, Mkurugenzi wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba.

Mkurugenzi wa Airtel amewanominate Exim Bank, City Bank na Standard Chartered Bank kujiunga na kampeni hiyo ambayo kiwango cha mchango kimetajwa kuanzia $100,000.

Kwa mujibu Sunil Colaso, Airtel itatoa shilingi 50,000 kwa member wa timu yake atakayekubali hiyo challenge ili pesa hizo ziende katika mfuko wa kusaidia mapambano dhidi ya fistula nchini.


Fistula Ice Bucket Challenge imenzishwa na Airtel Tanzania kufuatia kampeni maarufu ya marekani ya kuchangia utafiti wa ugonjwa wa ALS iliyopewa jina la #ALSIcebucketChallenge.
Previous Post Next Post