Roma aeleza jinsi mashabiki walivyoipokea collabo yake na Bob Junior na Comment za Mashabiki zinavosema

Baada ya kufanya Collabo ya Roma na Bob Junior iliyozaliwa kutokana na utani wa soka imekuwa moja kati ya mada zilizozungumziwa jana huku mashabiki wakitoa maoni tofauti kuhusu ngoma yao ya ‘Maumivu’.



Akionge na Times Fm, Roma ameelezea jinsi anavyoichukulia ngoma hiyo ambayo baadhi ya watu walionekana kumpinga kwa kufanya na Bob Junior wanaesema hukata mauno.


“Nairank katika asilimia kubwa sana za juu though ina siku moja tangu itoke kwa sababu officially tumeirelease jana. Na credit yangu naitoa kwa sababu ya comments ambazo nazipata. Katika comments 44 nakuta comments zinaonesha kuwa disappointed lakini zilizobaki zote zinakuwa nzuri. Na hiyo nimeizoea tangu nimeanza muziki wangu. Sijawahi kupokelewa positive tu. Watu wanashangaa hiyo collaboration jinsi ilivyotokea na kusahau kwamba wapo wasanii wengi tu wa nyuma waliwahi kufanya collabo na wasanii wa kuimba, Roma sio mtu wa kwanza.

“Nimeona hata jana katika mtando wa Facebook nikapata comments kama 237 hivi, kati hizo comments ni comments 33 zimepinga lakini zilizobakia zote wanasema muziki mzuri, ngoma kali na tumeielewa. Kwa hiyo unaweza kuona hapo jinsi ambavyo watu wameipokea katika kiwango kizuri.”
Previous Post Next Post