Rais Jakaya Kikwete amesema kinachojadiliwa kwenye bunge maalum la katiba si kinyume na rasimu ya katiba kama ambavyo inadaiwa na baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba hasa kutoka vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi.
Wajumbe hao ambao pia wamo kwenye Umoja wa katiba ya wananchi-UKAWA walisusia mjadala uliokuwa unaendelea kwenye bunge maalum la katiba na kutoka nje April 16 mwaka huu.
Rais kikwete amesema hayo jana wakati akitoa hotuba yake ya mwisho wa mwezi kupitia vyombo vya habari.
“Yapo madai mengine yanayotolewa na kuenezwa na wabunge waliosusia Bunge Maalum ya Katiba kwamba kinachojadiliwa bungeni sio rasimu ya tume ya mabadiliko ya katiba. Na ndio maana wanaweka sharti la kujadiliwa rasimu ya tume ya Jaji Warioba ndipo warudi Bungeni. Madai haya nayo yananipa tabu kuyaelewa.” Alisema rais Kikwete.
Ameeleza kuwa UKAWA walishiriki kwa ukamilifu katika kutoa maoni yao kama wachache na ufafanuzi wa maoni yao.
Aidha Rais kikwete amekanusha tuhuma zinazomkabili za kuvuruga zoezi la mchakato wa kupata katiba mpya.
“Mimi nadhani huenda katika kamati yamefanyika mabadiliko ambayo hayakuwapendeza. Kama hivyo ndivyo wawe wakweli kuhusu jambo hilo. Kuliko kusema mambo yasiyowakilisha ukwei halisi wa rasimu iliyojadiliwa. Kuhusu madai kuwa mambo yalikuwa yanakwenda vizuri na kwamba hotuba yangu ndio iliyavuruga, napenda kusema wazi kuwa lawama hizo nazo hazina ukweli wowote. Ni madai yasiyokuwa na msingi.”
Msikilize hapa:
Source:Times