Picha: True Love to the END, Wanandoa waliofariki pamoja baada ya mapenzi ya mika 62

Tumezoea kusikia wakati wa kufunga ndoa watu wakila kiapo kuwa watapendana hadi kifo kitakapowakuta, kiapo ambacho kwa baadhi ya watu huwa kama neno lililozoeleka kwenye shughuli ya harusi na baadae wakavurugana bila kulijali neno hilo.


Don na Maxine wakiwa katika shughuli za kijamii

Hii ni tofauti kwa Don na Maxine Simpson, wanandoa waliokuwa wakiishi katika jimbo la Bakersfield, California nchini Marekani ambao wameweka historia ya kushangaza walipopoteza maisha kwa pamoja baada ya kuishi katika ndoa kwa miaka 62 bila kuachana wala kutengana.


Don na Maxine walipokutana 1952

Kwa mujibu wa BBC, wanandoa hao walikuwa wamelazwa hospitalini kwa sababu ya hali duni ya afya iliyotokana na umri wao mkubwa. Inaelezwa kuwa wanandoa hao waliaga dunia saa nne baada ya kushikana mikono na kuahidiana kuwa wataendelea kupendana hata kifo kitakapowakuta.

Don na Maxine kabla ya kulazwa hostalini




Don na Maxine wakiwa hospitalini

Muda mfupi baada ya Maxine kufariki na mwili wake kuondolewa katika chumba walichokuwa wamelazwa pamoja, mumewe Don alifariki pia saa nne baadae kutokana na uchungu mkubwa na mshituko wa kuondokewa na mpenzi wake.



Mjukuu wake aliyetajwa kwa jina la Melissa Sloan, aliiambia KERO-TV kuwa babu yake alimpenda sana Maxine tangu walipokutana mwaka 1952 akiwa bindi mdogo katika mashindano ya Bowling.



“Babu yangu alikuwa anatamani kuishi na nyanya yangu na hata baada ya wawili hao kuanza kuugua kutokana na umri wao mkubwa waliwaomba wasimamizi wa hospitali walimolazwa wasiwatenge.” Alisema Mellisa.



Hadi mauti ilipowafika, Don aliwakuwa na umri wa miaka 90 na mkewe alikuwa na miaka umri wa miaka 87.



Don na Maxine wakiwa na watoto wao wawili

Kama watu hukutana ahera na maisha yakaendelea kama kawaida, wawili hao bila shaka watayaamishia mapenzi yao ahera penye amani ya kudumu.
Previous Post Next Post

Popular Items