Picha: Huyu ndiye mama mzazi wa Sylvester Stallone 'Rambo' Mcheki hapa akifanya mazoezi ya kubeba vitu vizito

Kibongobongo sidhni kama unaweza kukuta Bibi wa umri wa miaka 92 na zaidi akifanya mazoezi kama haya ya kubeba vitu vizito kwani wengi kwao ni mzigo na maumivu pia, kwenye Expandables, bila shaka ulipata kumuona Sylvester Stallone na katika kumtazama tua uanajua kwamba  umri wake umekwenda huku akiendelea kutisha kama bado ni kijana mdogo. Sasa utamshangaa zaidi mama yake mzazi, Jackie mwenye miaka 92 anaeamini umri sio kikwazo.

Bibi huyo ameendelea kufanya mazoezi ya viungo licha ya kuwa na umri mkubwa na hata anapokuwa gym hubeba hadi vyuma vyenye uzito huku akisaidiwa kwa ukaribu na watu.


Bibi Jackie bado anavaa Mini-Skirt, na kupaka make up kama wanavyofanya wasichana warembo wenye umri mdogo.

“Hollywood wanahofia umri, lakini nadhani wazee ndio wanakuja. Nadhani umri wa mwanamke wa kati unarudi. Wote tungependa kufika kule, kufika kule kama mimi. Sio kwenye kiti cha kukusaidia kutembea, wala kuwa kwenye kitu maalum cha kutunzwa.” Amesema mama Rambo.

Tazama picha hapa..





Previous Post Next Post

Popular Items