Nilimshuhudia mke wangu akijifungua , Ndio sababu nikatunga Nani kama Mama ' Christian Bella'

Mwimbaji wa dansi, Christian Bella ameeleza kuwa alimshuhudia mkewe akijifungua, kitu kilichomfanya aandike wimbo wa ‘Nani Kama Mama’ aliomshirikisha Ommy Dimpoz.



Christian Bella ambaye ni kiongozi wa Malaika Band ameeleza hayo wakati akiongea na gazeti la Mwanaspoti.

“Mwaka 2012 nilienda Sweden kwa mke wangu ambaye alikuwa anajifungua hivyo nililazimika kuwepo ili kushuhudia mtoto wangu akizaliwa .Nilishuhudia kila kitu na sasa nina watoto wawili wa kiume Jordan (7) na Hance (2).” Amesema Christian Bella.

“Niliamua kutunga wimbo huu baada ya kushuhudia hatua zote mke wangu alipojifungua, kiukweli mwanamke anatakiwa kuheshimika tofauti na wanavyowachukulia, hapo ndipo niliona kuna haja ya kuimba wimbo wenye ujumbe huu.”
Previous Post Next Post