Nicki Minaj avunja rekodi iliyowekwa na Michael Jackson....

Mwimbaji wa Kundi la Young Money,Nicki Minaj amevunja rekodi iliyowekwa na Michael Jackson ya kuwa na nyimbo nyingi zaidi kwenye chart ya billboard.



Akiwa na wimbo wake mpya, Anaconda ambao umeshika nafasi ya 19, Nicki Minaj amempiku hayati Michael Jackson ya kuwa na nyimbo 50 kwenye chart ya Billboard Hot 100. Kwa mujibu wa Mtandao wa Yahoo Music, muimbaji huyo sasa amefikisha nyimbo 51 zilizowahi kushika chart hiyo.

Kupitia Instagram, Nicki ameandika: ‘Made history today. I didn’t even know I was tied with Michael Jackson with 50 Hot 100 entries on Billboard. Anaconda makes 51 and now I’m tied with Rod Stewart. God bless, and thank you.’
Previous Post Next Post