MixTape: Rapper Mkongwe kutoka Arusha kwenye gemu ya HipHop Tdx Wangex ameachia Mixtape yake mpya ya 'City to City'

Muimbaji Mkongwe kwenye gemu ya Hip Hop kutoka arusha 'Tdx Wangez' utaweza kumkumbuka katka ngoma hii aliyofanya na Linex  na katika video yake hii mpya ya njoo kwa mjanja , sasa ameachia mixtape yake mpya ya city to city mixtape hiyo imebeba jumla ya ngoma 20 zilozobeba ujumbe tofauti.

Akiongea na Bongo61 Tdx Wangex alisema ;  'Kwa wadau wangu wote na wapenda Hip Hop hii ni  Mixtape yangu ya kijanja iliyokuwa inapikwa kwa muda mrefu sasa imekamilika na iko tayari kwa ajili ya wewe mdau kuweza kuisikiliza. City to City Nixtape ni mixtape inayoelezea Maisha Halisi ya Mtanzania katika Nyaja tofauti, Katika Mixtape hii kuna ngoma takribani 20 kwa ajli yako wewe mdau wa Tdx Wangex sasa ni muda wa kuwa na Mixtape yako upate kusikia nini nimefanya katika mixtape hiyo kwani utapata kusikia sauti tofauti mbali na Tdx Wangex

Sikiliza intro inayopatikana katika Mixtape hiyo



Tdx wangex akuishia hapo tu aliiambia Bongo61 ;Hii ni katika kukuletea wewe shabiki wangu kitu kipya masikioni mwako, Jipatie nakala yako sasa kwa bei nafuu ya Tsh 5000 tu Mkoa hadi Mkoa tuwasiiane na Mixtape ya City to City itakufikia

Mbali na hapo Tdx Wangex aliwahukuru wadau woote waliofanikisha mpaka kutokakwa mixtape hiyo

'Natanguliza Shukrani zangu za dhati kwa wadau na wote waliofanya mpaka mixtape hii kutoka.
Kwa mashabiki wangu wote Support yenu katika kusupport Tanzania Hip Hop Movement ni muhimu'


Mawasiliano:  +255 715 33 44 02 - #Tdx Wangex


Facebook Tdx Wangex
Instagram : TdxWangex1
Previous Post Next Post