Linex apanga uzinduzi wa video ya ‘Wema kwa Ubaya’ urushwe live kwenye TV

Msanii wa muziki, Linex Sunday anatarajia kufanya uzinduzi wa video yake mpya ya ‘Wema Kwa Ubaya’ ambapo uzinduzi huo amepanga urushwe live na EATV pamoja na Clouds TV.



Linex ameiambia alisema katika video hiyo watanzania watasikia maneno ya Zitto ambaye ameshirikishwa.

“Ni gharama sana kulipia ila itawezekana,” amesema Linex. “Tunataka kila kitu kiwe live ili na wateja wetu wa mikoani wapate kuona nini kinaendelea. Clouds TV tayari wapo confirmed bado tusubiria EATV. Kwahiyo kwetu sisi tumeplan iwe live Clouds TV na EATV. Ilikuwa ifanyeke hivi karibuni lakini tunasubiri kidogo kuna mambo bado yanawekwa sawa. Kama bado tupo kwenye mvutano na baadhi ya wadau wangu wengine wanasema ifanyike Mlimani City wengine Escape 1. Zitto kuna maneno ambayo ameyatoa mwishoni mwa video, ni maneno ambayo naweza sema ni makubwa sana.”
Previous Post Next Post