Haya ndiyo majibu ya Aunt Ezekiel kwa Diamond Platnumz kuhusu marafiki wa Wema ‘wapenda anasa’

Aunt Ezekiel ambaye ni Muigizaji wa filamu nchini, na rafiki wa karibu wa mpenzi wa Diamond Platnumz, Wema Sepetu amezungumzia kauli ya Diamond aliyotoa hivi karibuni kuwa mpenzi wake ana marafiki wapenda starehe na anasa.


Aunt alisema..

“Diamond alivyoongea pale hakunitaja jina, kwahiyo nikisema kwamba aliongea kwa sababu yangu nitakuwa muongo. Yeye aliongea kwa niaba ya watu ambao wako na Wema, hata kama angekuwa amenitaja jina sidhani kama angeongea kwamba yule mtu anafundishwa,” amesema Aunt. “Wema ni mtu mzima anaishi mwenyewe na ana maisha yake sidhani kama ni mtu wa kufundishwa. Wema ni mtu ambaye ana maamuzi yake, watu hawajui kuna wakati wa kazi na kuna wakati wa kuspend maisha. Kwahiyo mimi na muda wangu wa kazi na nina muda wangu waku spend.”

“Sihitaji kuangalia kuna mtu anafuatilia maisha yangu kwamba eti nakuwaga na Wema. Hawanisaidii chochote. Nachotakiwa kuangalia nafanya kazi zangu na maisha yangu yanaenda mbele na sitaangalia watu wanasema nini. Mimi nina kazi zangu. Sijui kama Wema kama anahitajika kubadilika kwa sababu Diamond ndiyo anajua mapungufu ya Wema na Wema anajua ya Diamond.”

Kwa upande mwingine muigizaji huyo amesema anakuja na filamu yake mpya iitwayo ‘Mwajuma Nipe’.
Previous Post Next Post