AY kuachia ngoma aliyomshirikisha Sean Kingston, kuiachia kimataifa

Msanii AY anatarajia kuachia nyimbo mbili za kimataifa mwezi November mwaka huu. Miongoni mwa nyimbo hizo ni pamoja na ule aliomshirikisha Sean Kingston.



Akiongea na kituo cha redio cha Nuru FM cha Iringa hivi karibuni, AY alisema miezi ya hivi karibuni amekuwa akiachia nyimbo kwaajili ya soko la ndani ukiwemo ‘Asante’ na wimbo mwingine atakaoutoa hivi karibuni. Alidai kuwa baada ya nyimbo hizo ndipo atakaporejea tena kwenye nyimbo kwaajili ya soko la kimataifa.

Katika hatua nyingine AY amekiambia kituo hicho kuwa yeye na Diamond watawekeza kufanya video ya wimbo mpya wa Chidi Benz, ‘Mpaka Kuchee’ walioshirikishwa.

“Watu wategemee video nzuri ya Chidi Benz,” alisema.
Previous Post Next Post