Hatua dhidi ya Ebola kuimarishwa

Kiwango cha maambukizi ya virusi vya Ebola yanaonekana kuwa makubwa kuliko ilivyokadiriwa, linasema Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, wakati ambapo idadi ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo ikiongezeka kufikia 1,069.

Shirika la Afya Duniani limesema wafanyakazi wake wameshuhudia kwamba idadi ya wagonjwa na vifo vinavyoripotiwa haionyeshi ukubwa wa tatizo.



Mlipuko ulianzia Guinea mwezi Februari na tangu wakati huo ugojwa wa Ebola umesambaa katika nchi za Liberia, Sierra Leone na Nigeria.WHO limesema "hatua za ziada" zinatakiwa.

Hata hivyo, WHO wanasema hatari ya maambukizi ya Ebola wakati wa kusafiri kwa ndege bado iko chini, kutokana na ugonjwa huo kutokuwa wa kuambukiza kwa njia ya usafiri wa anga.

Kwa matokeo hayo, Shirika la Ndege la Kenya, Kenya Airways, limepinga shinikizo la kutaka kusitisha safari za ndege zake katika mataifa yaliyokumbwa na Ebola huko Afrika Magharibi.

Ugonjwa wa Ebola unaambukiza kwa njia ya kugusana na majimaji ya mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo

Mwandishi wa BBC Ishaq Khalid anasema ujumbe mfupi wa simu za mkononi ulianza kusambaa nchini Nigeria mwishoni mwa wiki iliyopita ukiwataka watu kunywa na kuoga maji ya chumvi kama njia ya kuzuaia maambukizi ya virusi vya vya ugonjwa wa Ebola, ambao hauna tiba wala chanjo.

Ingawaje waziri wa afya wa Nigeria alipinga uvumi huo, watu wengi wamelazwa hospitali baada ya kunywa maji ya chumvi.

Ebola inambukiza kwa kugusana moja kwa moja na maji maji ya mwili wa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo.

Dalili za mwanzo za ugonjwa wa Ebola zinaweza kusababisha damu mgonjwa kutokwa damu sehemu zote zenye matundu katika mwili kama vile machoni, fizi na kuvuja damu ndani ya mwili kunakoweza kusababisha viungo vya ndani ya mwili kushindwa kufanya kazi.

Source: BBC
Previous Post Next Post