Diamond Platnuzm na Wema Sepetu waamua kufikia hapa, baada ya Miaka minne

Ni miaka minne imepita hadi sasa toka mahusiano yao yalipoanza, unaweza kusema kati ya vitu ambavyo wamepitia wawili hawa(Wema na Diamond ), ni misukosuko ya hapa na pale, moja ya vitu ambavyo vimeweza kuweka mahusiano yao yasimame imara hadi hivi sasa. Safari ya miaka minne mbali na kuwa na vikwazo vingi, ikiwemo kuachana na kurudiana mara kwamara, kuumizana wenyewe kwa wenyewe katika safari yao, Wema Sepetu alitokea kufunguka kuwa hivi sasa inatosha, na haina budi kutulia.


Wapenzi hao maarufu sana, ikiwa ni moja ya celebrity couple yenye nguvu zaidi, ikiwa kila mmoja wao ana fanbase kubwa sana(mashabiki), walitokea kufunguka mapema mwaka huu kfikia kwenye uamuzi wa kukaa chini na kupanga mipango makini sana ya kuwa mume na mke, hii ni moja ya hatua ambayo si watu wengi, au wasani wengi wameweza kufikia hadi hii leo, mbali na watu wengine kutabiri kuwa, mapenzi yao hayatadumu, ila vitendo vyao na malengo yao katika kujipanga hivi sasa inaonyesha kuwa watabiri hao wataendelea kusubiri sana.



Wema alitokea kusema kuwa bila nguvu ya mashabiki wake ambao anawapenda sana, hii leo yeye na Diamond Platnumz wasingekuwa hapa sehemu hii walipo katika maisha ya mahusiano yake, Wema sepetu alizidi kufunguka na kusema kuwa inakuwa inatia moyo kwa shabiki mtu ambaye hata hujawahi kukutana nae anaweza kuonyesha mapenzi makubwa kwake, na kuweza kuwa katika sehemu kubwa ya maisha yake, hii ni kutokana na mara nyingi ugomvi wowote utokeapo kwenye mitandao, mashabiki wake ndio wanamalizaga na kutuliza ugomvi huo, hadi kufikia kipindi wema kusemekana kuwa huwa anawatuma mashabiki wake, jambo ambalo si kweli bali ni mapenzi yao kwake kwani wako teyari kupigana kwa ajili yake.
Previous Post Next Post

Popular Items