Diamond Platnumz awajibu wale #BringBackourWema

Kupiti Instgram kuna mambo mengi yamekuwa yakiendelea  jana tulipost habari inayosema kuna kikundi cha mashabiki wanajiita #BringBackOurWema 

Mashabiki hao wanaamini kuwa Diamond anampoteza Wema na amekuwa akitumia umaarufu wake (Wema) kujidhatiti zaidi yeye huku Miss Tanzania huyo wa zamani akiendelea kudidimia.

Hivi ndivyo mmoja wa mashabiki hao alivyoandika :

@diamondplatnumz mambo vipi? Sisi mashabiki wa @wemasepetu tunakuomba umsaidie Wema kama yeye anavyokusaidia. Labda niseme kwa uwazi bila woga kwamba mahali ulipo kimziki umefika sababu ya Wema. Wengine hatukuwa mashabiki wako lkn sababu ya mapenzi kwa Wema tukajilazimisha kukupenda tu… so unajua vema bila wema we mziki huna!



Diamond kupitia ukurasa wake wa instagram. aliwajibu mashabiki hao ,Ujumbe huo unaonekana unaenda kwa msanii fulani japokuwa hakuweka wazi ni msanii gani. Diamond aliweka post hii na baada ya muda mfupi aliifuta lakini maneno yote yalikuwa yanasomeka hivi.

Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu… kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe…

Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi…. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng’ombe wake Kwenye Maji safi….ila yeye ng’ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!!

Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!… leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!….Mxieeeeeeeew!�� Kama nimekuchefua Lamba ndimu Usitapike”.
Previous Post Next Post