Baada ya taarifa za Ebola Kuingia Tanzania, Hii ndio kauli ya Wizara ya afya

Zile tetesi za Ugonjwa wa Ebola kuingia Tanzania, zimekanushwa na Wizara ya afya, kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya wa Tanzania Seif Rashid amesema, wagonjwa hao waliohisiwa kupata maambukizo kutokana na dalili za awali, ni wa kutoka Benin na Mtanzania, lakini vipimo vimeonesha hawana maambukizo hayo.




Waziri Seif Rashid amesema kuwa tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo ikiwa ni kauli iliyotoka baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliohisiwa.

Kupitia ukurasa wake wa facebook, Waziri Seif amesema vifaa maalumu vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia wagonjwa vimewekwa pia huku wizara ya afya ikiongeza uwezo wa kufanya uchunguzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao wasafiri wengi kutoka nje huutumia.
Previous Post Next Post