Watanzania wataka bangi ihalalishwe, ni baada ya kuitumia kama mboga

Watu wa Makete hutumia mbegu za Marijuana kukaangia chakula tangu zamani. Huku harakati za kutaka matumizi ya Bangi kuhalalishwa zikishika kasi katika sehemu mbali mbali duniani, Tanzania haijaachwa nyuma.


Wanakijiji katika wilaya ya Makete , mkoa wa Njombe Kusini Magharibi mwa Tanzania wanataka serikali iweke sheria ambayo itaweza kuhalalisha matumizi ya mmea huo.

Wanakijiji hao zamani walikuwa wakitumia mbegu za mmea huo kukaanga na chakula lakini siku hizi wanalazimika kuzitumia kwa usiri mkubwa wakihofia kukamatwa na polisi.


Mwenyeketi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Daniel Okoka amesema matumizi ya Bangi katika wilaya hiyo hayajaanza leo, tangu zamani watu kitamaduni walikuwa wakitumia Mbegu za Bangi kukaanga na chakula.

Na kama mmea huo ungekuwa na tahri kubwa kiafya, basi watu wengi wilayani humo wangekuwa vichaa.


Chanzo: BBC
Previous Post Next Post