Teknolojia: LG kutengeneza TV nyembamba kama karatasi zenye uwezo wa kuviringishwa

Kampuni ya LG Electronics ya Korea kusini imetangaza kuwa iko mbioni kutengeneza TV zenye wembamba kama wa karatasi, na ambazo zinaweza kukunjwa au kuviringishwa bila kuharibika.


Kampuni hiyo imesema kwa sasa inatengeneza toleo lenye ukubwa wa inchi 18 na kuongeza kuwa toleo la inchi 60 litaingia sokoni ifikapo 2017.

“We are confident that by 2017, we will successfully develop an Ultra HD flexible and transparent OLED panel of more than 60 inches, which will have transmittance of more than 40 percent and a curvature radius of 100R, thereby leading the future display market.” alisema Byung Kang, mmoja wa viongozi wa LG Display.
TV hizo zenye uwezo wa kukunjwa na kubebwa kirahisi zitakuwa na picha zenye ubora wa ‘Ultra HD’.

TV hizo pia zitakuwa ni ‘transparent’ pale zinapukuwa zimezimwa, kwa maana kwamba unaweza kuona upande wa pili kama kioo.
Previous Post Next Post