Stereo kuja na video ya wimbo ‘Usione Hatari’ july 11

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Stereo, kesho anatarajia kuachia video ya wimbo ‘Usione Hatari’ ambayo imetengenezwa na Adam Juma.


Stereo amesema baada ya kuachia video ya Usione Hatari atakaa siku chache na baada ya hapo ataachia tena wimbo ambao amefanya na Victoria Kimani.

“Mambo yameiva , video ya Usione Hatari itatoka ijumaa, nimefanya na Adam Juma next level, video ni nzuri wadau wasubirie vitu vizuri kutoka kwangu, pia nikitoa video ya Usione Hatari siku ya ijumaa, wiki inayofuata ninatoa wimbo wangu mpya iliyomshirikisha Victoria Kimani, unajua sasa hivi baada kumaliza chuo nimepata muda wa kufanya muziki wangu vizuri, kwaiyo wadau wakae wakisubiria mambo mazuri toka kwangu” Alisema Stereo.


Previous Post Next Post