Music: Izzo Bizness – Walalahoi (Prod. Duppy) +Lyrics

Hit maker wa Tumoghele Izzo Bizness ameamua kwenda hard na tofauti zaidi kwenye ngoma hii mpya ‘Walalahoi’ iliyotayarishwa na producer Duppy. Kwenye ngoma hii anayoimba kuhusu mambo mengi yanayotokea mtaani yanasababishwa na walalahoi, Izzo anaonesha uwezo wake wa Tongue Twist mtindo ambao anaonekana kumuudu haswaa. Kwa beat kama hii huwezi kuacha kutikisha kichwa chako kufuatiliza kicks, snare na baseline iliyocharazwa kwa ustadi





Mistari ya wimbo huu iko hapa....




WALALA HOI lyrics

Intro:
Walala hoi…Walala hoi…Walala hoi
Chorus:
Walala hoi sisi ndio Walala hoi (Walala hoi) x 4
moja haikai mbili haikai mbaya wako ni jirani babu (Walala hoi) x 4


Tunaunga unga maisha yetu ni safari bado tunataabika (Walala hoi) / tunakomaa maisha ni safari imani ipo bado sisi mbali tutafika (Walala hoi) / tumazaliwa kwenye njaa njaa imetulea sisi home mali hatujakuta (Walala hoi) / mama Yanga baba Simba upinzani babu ndani yani kila dakika (Walala hoi) / kupinda ni sheria usishangae huku kwetu mbona imeshazoeleka (Walala hoi) / hatujasoma dili chafu leta pesa babu hata iwe dili ya kuteka (Walala hoi) / tunaonekana hatuna maana tunatengwa kona zote twa dharaulika / majina yote sisi Vidampa wapumbavu wezi majambazi yote wametupachika / Rhumba kali wewe utadata/ soma pata ondoa shaka/ faster umenipata chafu tatu maisha karata/ maisha bondi kukosa na kupata / jela nyummbani hakuna kuogopa sheli tunamoka/ sisi machizi kama kaboka/ uchungu wa meno na kucha kamuulize Ulimboka /

Chorus:Repeat

Verse 2:


Roba za mbao mtaani ni nani kaleta? (Walala hoi) / kulogana logana tu bila sababu mtaani? (Walala hoi) / majungu fitina unafiki umbea na chuki? (Walala hoi) / kazi ngumu tunapigika lakini ujira ni mdogo babu (Walala hoi)/ toa kazi tumalize hatulazi kitu hapa sisi mwendo ni wa CHAP-CHAP/ kwenye Bar hatukai zetu vilabuni yes sisi mwendo ni MATAPU-TAPU / bila sababu tunakudiss tukijua umetuzidi sisi wala hatukukwepeshi / chuki roho mbaya jadi yetu Mungu hapendi lakini sisi tumerithi / kila time tupo simple watu wa Mingle mawazo yetu kwenye Bingo dr.Kingo ngoma zetu ni Segere na Msondo / sisi ndio wachezeshaji tuite Redondo / Rest in Peace James mtoto wa Dandu / hii game bado kwako japo upo kando / big brother the Chase muulize Nando / kama Zay-B vile watu wapo gado /

Chorus:Repeat
Outro: Walala hoi…Walala hoi…Walala hoi…Walala hoi x 3…hoi hoi hoi Walala … hoi hoi hoi Walala… hoi hoi hoi Walala.
Previous Post Next Post