Kupumua 'Kujamba; hupunguza mtu kupata magonjwa haya

Wanasayansi wanasema kunyamba ni afya, Kila mmoja wetu kwa wakati fulani huhisi kuvimbiwa na gesi nyingi tumboni.Suluhu ya pekee hapa huwa ni kujamba ili kupunguza gesi hiyo tumboni

Sasa Wanayansi katika chuo kikuu cha Exeter, nchini Uingereza, wanasema kuwa wamegundua harufu mbaya kama vile ya kujamba japo inachukiza kwa pua, ina manufaa makubwa kwa afya ya binadamu.

Wanasayansi hao wanasema kuwa harufu hiyo mbaya inaweza kuwa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo na akili na hata Saratani.



Gesi au harufu mbaya ambayo hutokana na chakula kinachosagwa tumboni mwako inaweza kulinda baadhi ya viungo vya mwili wako.

Ndio! athari ni kile ambacho unakidhania: Eti watu wanauchukulia utafiti huu kumaanisha kuwa harufu mbaya inayotokana na mtu kujamba inaweza kuzuia magonjwa fulani mwilini kama vile Saratani.

Utafiti huo uliochapishwa katika mtandao wa chuo kikuu cha Exter uligundua kuwa gesi hiyo inayojulikana kama Hydrogen Sulfide ambayo pia hupatikana katika Mayai yaliyooza, inaweza kuwa muhimu katika kutibu baadhi ya magonjwa.

“ingawa gesi ya hydrogen sulfide inajulikana kuwa na harufu mbaya na hupatikana katika Mayai yaliyooza pamoja na harufu ya mtu kujamba, hutengezwa mwilini na inawezekana kuwa tiba kwa magonjwa fulani, ”asema Daktari Mark Wood,Profesa wa chuo hicho cha Exeter.

Gesi hiyo ina athari mbaya ikiwa katika viwango vikubwa , kwa mujibu wa utafiti huo.

Watafiti wanasema licha ya harufu hiyo mbaya ya kujamba kuchukiza, ina uwezo mkubwa wa kupunguza uwezekenano wa mtu kupatwa na magonjwa kama vile, Saratani,Kiharusi, mshtuko wa Moyo na kuumwa na mifupa
Previous Post Next Post