Dully Sykes anasema imepita miaka miwili sasa hajawahi kupigiwa simu na promota yeyote nchini kwaajili ya kufanya show.
“Sijaitwa na promota miaka miwili sasa hivi, sijawahi kupigiwa simu na promota kwaajili ya show,” Dully alimuambia DJ Majay wa EFM jana.
Hata hivyo amesema kukosa show hizo ni kwasababu hajajiweka ‘cheap’. “Sababu sina shida ya kusema nimkubalie promota kwa milioni moja, milioni moja na laki tano anipeleke Mwanza wakati milioni mbili nikitaka wiki moja tu naipata kwenye kazi yangu,” alisema Dully ambaye wiki hii ameachia wimbo mpya, Togola.
Dully alisema show yake ya kwanza aliyoipata na kulipwa fedha nyingi ni ile aliyolipwa shilingi 50,000 na kudai kuwa kipindi anaanza muziki alikuwa akilipwa shilingi 15,000 au 10,000 kwa show za mikoani. Amesema fedha kubwa aliyowahi kulipwa katika career yake kwa show moja ni shilingi milioni nane.