Dudu Baya wawataka Ali Kiba na Diamond Kutengeneza Pesa, Beef sio issue!

Msanii Mkongwe Dudu Baya ametoa ushauri kwa wadogo zake Diamond Platnumz na Alikiba akiwaambia kuwa watambue nguvu yao na waitumie kutengeneza fedha pamoja na sio kuendekeza ugomvi.




“Ninachowashauri hawa wadogo zangu watulie chini wajitambue ni wasanii na usanii wao ni wa kutengeneza pesa, tena watengeneze hata tour ya amani wazunguke nchi nzima, wazunguke hata Afrika Mashariki na sio hizi beef,” rapper huyo mkongwe ameiambia AyoTV.

“Siku moja nilikua na Dully Sykes na Christian Bella alafu watu wakawa wanasema Diamond ooohhh sijui kashindaje tuzo saba, nikawaambia hivi ukiwa na akili timamu wimbo kama ‘my number one’ kila kona unayopita, video mpaka TV za kimataifa zinapiga Halafu leo unaweza video yako ya kijingajinga unategemea kuishinda ‘my number one’ …….Diamond alistahili kushinda hizo tuzo saba, mimi sikuona cha ajabu,”aliongeza.
Previous Post Next Post