Busta Rhymes ajiondoa YMCMB, aeleza sababu

Busta Rhymes ametangaza kujiweka kando la label ya YMCMB baada ya kufanya nao kazi kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

Busta ameweka wazi uamuzi wake wakati akifanya mahojiano na SiriusXM katika kipindi cha Sway in The Morning huku akitoa sababu kuwa ni kutoelewana katika masuala ya ubunifu.



Busta ambaye aliwahi kuingia katika label ya Dr Dre na kushindwa kudumu pia alisema hakuna tatizo hasi katika kuondoka kwake katika label hizo bali kutofautiana katika makubaliano wakati wa masuala ya ubunifu ndio chanzo kinachopelekea mengine kuibuka.

“Kitu ambacho ni sawa na Cash Money, nilikuwa pale kwa kipindi cha miaka miwili na fursa zilikuwa kubwa kwa kipindi hicho kwa sababu ya aina ya deal iliyokuwa iliyofanyika. Kwangu mimi, huu mradi na vyote nilivyojitolea…kurekodi albam kwa kipindi cha miaka mitano. Nilimpoteza Chris Lighty kuifanya albam hii, nilimpoteza baba yangu kuifanya albam hii. Kitu nilichokuwa naweka kwenye albam hii, sikubali kupotezea maono yangu kwa hicho.”

Busta alitangaza kujiunga na Cash Money November, 2011 lakini hajawahi kuachia albam akiwa nan a label hiyo.

Mwanzo wa mwezi huu aliachia wimbo aliomshirikisha Eminem ‘Calm Down’, na anajiandaa kuachia albam yake ya kumi inayoitwa E.L.E.2.
Previous Post Next Post

Popular Items