Baada ya Ukimya wa Muda Mrefu sasa Bushoke kurudi na Album Mpya

Ni muda mrefu toka Bushoke aachie ngoma mpya na kweli ashabiki wengi wamemmic na wanatamani kusikia kitu kutoka kwake, Hatimaye Hitmaker wa nyimbo kama Barua,Mume Bwege na Dunia Njia, Ruta Bushoke ambaye kwa sasa anaishi nchini Afrika Kusini, anatarajia kuachia wimbo mpya na album.



Bushoke alisema katika album hiyo amemshirikisha baba yake Mzee Max Bushoke aliyewahi kuwa mwanamuziki wa bendi ya Sikinde huku kwa sasa akifanya kazi ya utangazaji nchini humo.

“Album yangu mpya ambayo nimemshirikisha Baba Mzee Max Bushoke inaitwa Bushoke international Album,” amesema Bushoke.

“Nimemshirikisha katika nyimbo kama 3. Bado haijaisha. Ila nyimbo kama 8 zipo tayari Ukiacha ‘She Want It’ niliyofanya na Face off kutoka Uganda. Kwa sasa “Bwagamoyo” ndio nyimbo rasmi ntaitambulisha nimeimba peke yangu. Nimefanya katika studio inaitwa Tidy Production Cape Town, producer ni Danro. Na pia nimeshafanya video za ngoma kama tatu pamoja na hii ya Bwagamoyo.”

Previous Post Next Post