Young Killer aeleza kwa nini alipanda jukwaani na mama yake mzazi kwenye Kili Music Tour

Young Killer Msodoki, Mshindi wa KTMA 2014 aliwasurprise wakazi wa jiji la Mwanza baada ya kupanda jukwaani na mama yake mzazi katika show ya Kili Music Tour.



Rapper huyo ambaye Mwanza ni nyumbani kwao amekiambia kipindi cha The Jump Off cha 100.5 sababu iliyompelekea kupanda jukwaani hapo na bi mkubwa wake.

“Ilikuwa ni moja ya Surprise kwa sababu ujue toka siku niliyochukua tuzo nilishindwa hata kuongea, so bi mkubwa wangu alikuwa na mengi sana ya kuzungumza na mashabiki wangu wale ambao wamenifanya mpaka nimefika hapa.

“Kwa hiyo atayawakilisha wapi yale aliyokuwa nayo moyoni. So, nikaona nafasi pekee ambayo anaweza akafanya nikupanda nae stejini na kuongea dukuduku lake lote na kuwapongeza mashabiki waliokuwa wananikubali na kunisapoti mpaka nikafika pale.”
Previous Post Next Post