Wasanii wengi wa bongo hufuata upepo, mwana FA afunguka

Mwana FA ni msanii ambaye alianza kumtaja mweusi G Nako kama msanii wa anaefanya viitikio bora zaidi vya hip hop kabla hatujasikia akiitikia vyema kwenye wimbo wake ‘Mfalme’.

Baada ya kutoka Mfalme na kukubalika sana, tulimsikia G Nako akibadili mawazo na kuanza kulipisha fedha wale wanaotaka awafanyie chorus kwa kuwa foleni ilikuwa kubwa sana.




Mwana FA ametoa mtazamo wake kuhusu uamuzi huo wakati akiongea na The Jump Off ya 100.5 Times Fm inayoongozwa na Jabir Saleh aka Kuvichaka.

“Mimi nafikiri kuna vitu vingine vinakufanya unakuwa dog father, kwa sababu G-Nako hakuanza kuwa mbaya kwenye Mfalme, hajaanza kuwa mbaya juzi. G Nako amekuwa akifanya muziki mzuri muda mrefu lakini nafikiri spotlight ilikuwa haimuangalii. Watu walikuwa hawapay enough attention naweza kusema.” Amesema Mwana FA.

Ameeleza kuwa watu walianza kuwa makini zaidi na G Nako baada ya kumsikia akifanya kitofauti zaidi kwenye Mfalme na ndipo wengi wakaanza kumkimbilia, suala ambalo analiita kufuata upepo.

“Lakini sio hivyo, unajua haijalishi unafanya ngoma na nani. Kinachomatter ni kwamba ngoma yenu itatoka namna gani. Majina yanaweza kukubeba kiasi fulani lakini muziki mzuri ndio kitu cha msingi. Kama mimi ningekuwa nafuata upepo hufikiri kama mimi ningeenda kufanya Diamond sasa hivi. Kwa sababu sio kwamba siwezi kumfuata Diamond akaja kufanya ngoma yangu lakini nafiriki kwamba inabidi nitoke kwenye angle ningine kama msanii na ndio maana nikafanya na Diamond.”

Mwana FA amesema hata kama watu wangeambiwa wataje watu watano wa kufanya nao featuring kwenye Mfalme kuna uwezekano mkubwa kwamba jina la G Nako lisingetajwa lakini yeye aliona mbali.

Video ya Mfalme itafanyika nchini Kenya chini ya muongozaji Kevin Bosco Jr na wataanza kushuti wiki ijayo.
Previous Post Next Post