Uganda yawekewa vikwazo na Marekani baada ya kupitisha sheria ya kupinga ushoga

Baada ya Uganda kupitisha sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja mwezi Ferbruari mwaka huu, serikali ya Marekani imeiwekea vikwazo nchi hiyo kwa madai kuwa inakiuka haki za binadamu.


Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Afisa Uhusiano anayesimamia maswala ya usalama katika Ikulu ya whitehouse, Caitlin Hayden imesema vikwazo hivyo vitajumuisha kuwapiga marufuku wanaharakati waliopigia debe sheria hiyo kupitishwa kutoingia Marekani.

Miradi itakayoathirika na marufuku hiyo ni pamoja na ushirikiano na polisi wa Uganda na Wizara ya Afya.

Aidha msaada kwa miradi iliyoanzishwa kwa usaidizi wa marekani pia utapunguzwa mbali na kufutiliwa mbali kwa mazoezi ya kijeshi kati ya majeshi ya uganda na yale ya Marekani.

Mbali na Marekani, mataifa mengine ambayo tayari yamesitisha kutoa misaada kwa Uganda ni pamoja na Uholanzi, Sweden, Denmark pamoja na Norway.

Previous Post Next Post