Rihanna ajifunza kulea mtoto!

Rihanna hivi sasa ameonesha upande wa pili wa maisha yake kama mwanamke wa kawaida anaetamani kuwa mama wa mtoto tofauti na maisha ya ustaa na kula bata.



Mwimbaji huyo hivi sasa ameonekana kutumia muda wake mwingi kukaa na kichanga wa mdogo wake huku akimuonesha malezi yote kama mama yake mzazi kasoro kumnyonyesha.

Mdogo wake ameamua kuwapa jina la utani Rihanna na mwanae ‘Pinky and the bail’ na anasema sababu kubwa ya kuwapa jina hilo ni kuwa wao hupenda kuangalia cartoon badala ya kombe la dunia na wanalala pamoja.

Huenda Rihanna akayazoea maisha ya mama na kuamua kuwa kama Ciara, Lil Kim na Beyonce ambao wao tayari ni akimama.
Previous Post Next Post