Picha:Mabanda ya wafanyabiashara wa soko la Karume yateketea kwa moto

Maafa! Moto mkubwa umetetekeza kabisa soko kubwa kabisa la mitumba la karume jijini Dar es Salaam usiku wa Jumatano, na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara wote wa soko hilo.




Baadhi ya mabanda yakiteketea kwa moto

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wamedai moto huo ulianza kuteketeza mabanda hayo majira ya saa 4 usiku, huku wakijaribu kutafuta msaada kuuzima bila mafanikio yeyote.



Wazima moto walifanikiwa kuudhibiti moto uloweza kufikia karibu na kiwanda cha Breweries, lakini haujasababisha hasara yeyote katika nyumba za jirani wa soko hilo kwa mujibu wa mwandishi habari wa Raia Mwema Mbaraka Islam alipozungumza na Sauti ya Amerika.




Anasema hakuna kibada cha biashara kilichosalimika na hakuna mtu aliyefanikiwa kuokowa mali yake. Mfanya biashara Wilson magembe anasema amepoteza kila kitu na ilikuwa vigumu kuweza kuchukua bidhaa zao kwa sababu moto uliwaka kwa haraka sana.
Previous Post Next Post