Majibu ya Monalisa kwa wanaodai alichukua pole zisizo zake kufuatia msiba wa George Tyson

Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa ambaye alifunga ndoa na marehemu George Otieno Tyson amewajibu baadhi ya watu wamekuwa wakisema alichukua pole za msiba asizostahili.

Monalisa ameshindwa kuvumilia na kuyatolea majibu madai hayo kupitia Instagram kwa lengo la kuweka mambo sawa:


“Let me clear the air. Ni hivi, pamoja na ujinga wote tuliofanya mimi na George ktk maisha yetu, kwa macho ya binadamu utasema alikuwa na mke mwingine..but kwa macho ya kimungu mimi ni mke halali wa George Otieno Okumu aliyelala.anayesema mke wa Tyson alijifungia ndani mimi nikawa nachukua pole zisizo zangu.dah! kwanza wanawake walikwua wawili ndani sio mmoja. Na wote walijifungia ndani. Kwa nini? ni wakristo na wanaijua dini. Waombolezaji waliokuwa wakinipa pole mimi, ni kwaninini? Jiulize kabla ya kuropoka halafu wewe ni mwanamke kuna siku yatakukuta…nilienda kutimiza wajibu wangu kama mke, ningelia peke yangu kwetu mgesema sana, n imekaa msibani naambiwa nachukua pole za bure. Wacha nikukumbushe maandiko …alichokiunganisha Mungu?....Kilichofungwa duniani?....nikupende nikutunze hadi kifo?.....sasa kifo kimetutenganisha. Siku ya mwisho unadhani George ataitwa na nani? Pamoja na mambo yake yote wacheni nimlilie he was a good father kwa Sonia wangu esp miaka mitano ya mwisho wa uhai wake. Achene nimlilie he was my best friend 1998-2014. Nimeshare nae kitanda 2000-2006. nitakuwa mtu wa aina gani nisiwe na uchungu? Ukiona mwanamke mwenzio kaishindwa ndoa usimcheke jua kuna sababu…na ni fundisho kwa wanaochukua waume za watu wote mjini. Mme akiumwa huwa anarudi kwa mkewe. Na akifa? Na for ur info, msianze anajifanya mke ss hivi ili apewe mali…Sonia ni mali kubwa sana aliyoniachia am so happy. Waache wao wanaolilia kupewa pole wapiganie. Mwenyewe alitafuta kafa kaziacha sembuse tuliobaki? Niacheni nimlilie, waacheni fans wangu walie na mm.

Monalisa aliongeza post ya pili kuhitimisha alichokitoa moyoni:

“Yatosha...ila napenda kuwashauri tu hata siku moja usicomment kitu ambacho hukijui,ni mbaya sana.na mtu usikurupuke kucomment kabla hujasoma na kuelewa vzr.ila ndo watanzania tulivyo,watu wanakujua kuliko unavyojijua..na siku zote mwanamke akifanya kinaonekana kibaya kuliko mwanaume.nyie mnaongea ongea tu laiti mngeujua ukweli,ee Mungu nipe subra.ile post naifuta maana naona nawapa watu ela na kik za bure.pole kwa wote waliokereka na pole kwa wote mnaoomboleza pamoja nasi.Pumzika kwa Amani Baba Sonia..”
Previous Post Next Post