Lucci amuuliza Rais Kikwete Maswali kuhusu uamuzi wa kumleta Usher Tanzania

Uamuzi wa mheshimiwa Kikwete kumleta Tanzania mkali wa R&B Duniani, Usher Raymond na Terrence J ili kuendesha semina kuhusu Sanaa ya muziki na filamu na mambo mengine umezua maswali mengine kichwani kwa mtayarishaji wa muziki, Lucciano Tsere aka Lucci.




Kupitia Twitter, Lucci ameandika tweets zenye maswali kadhaa kwa mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Hongera kwako mheshimiwa rais Kikwete kwa juhudi unazofanya kwa ajili ya wasanii wa taifa letu, hata hivyo; nina walakini kidogo.”





“Ni kitu gani ambacho wasanii tumefanya kwa elimu tuliyoipata mara kwa mara kutoka katika taasisi zetu kama BASATA na COSOTA?”

“Kuna msemo ‘yule mwenye kuaminika kwa kidogo hudhaminiwa kikubwa’…Je, Mheshimiwa Jakaya Kikwete, tumekuwa waaminifu kwa kidogo?”
Previous Post Next Post