Davido alichowai kufanyiwa na Baba yake Mzazi atoweza kukisahau

Katika maisha, mara nyingi mambo mengi haswa yale ya maendeleo unapoanza kufanya unakutana na vishawishi na vikwazo vingi, watu wengi hukata tamaa pale wanaposhindwa kukabiliana na vishawishi hivyo, 




haswa pale katika ndoto za mtu akijaribu kukamilisha jambo fulani afike mahali anapotaka, hii imetokea kwa watu wengi sana, ila mmoja wapo ni huyu msanii Davido kutoka nchini Nigeria,ambaye kwa hivi sasa jina lake siyo lazima uingie google kumjua, kila mtu namfahamu fika kama King wa Skelewu.


Davido mwenyewe aliwahi kukiri kuwa hatosahau alichowahi kufanyiwa na Baba yake mzazi, kama walivyo wazazi wengi wa hapa Bongo, pale wanapoona mtoto ananza kujihusisha na maswala ya muziki, Davido yalimkuta hayo hayo, 



Baba yake alikuwa anampinga vikali katika kujihusisha na maswala haya ya muziki, akiwa bado anatoka(underground) inasemekana kuwa, baba yake alikuwa anachukizwa na mambo aliyokuwa anayafanya na alikuwa hataki kabisa kusikia mambo ya kujihusisha na muziki, huku Davido kwa kujiamini aliendelea kufwata ndoto zake mwenyewe na kupita pingamizi hizo kutoka kwa baba yake mzazi.


Hivi sasa Davido ni msanii mkubwa sana maarufu anayemiliki majumba na magari ya kifahari kupitia muziki huo huo, na kwa jinsi inavyoonekana, walishayasamehe yeye pamoja na baba yake mzazi nakuyaacha yapite, sababu ameonekana mara nyingi akiwa na baba yake katika picha, ingawa baba yake ni mtu tajiri sana, ila umaarufu wa Davido haukutegemmea hela za baba yake, kutokana n kujiamini katika kipaji chake mwenyewe ambacho ndicho kilichomletea mafanikio ambayo hadi leo Davido kujulikana karibia Dunia nzima, haswa kwa hit single yake ya skelewu.

Previous Post Next Post