Ay na Faraja Kotta wachaguliwa kuwa Mabalozi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto, UNICEF, limemteua msanii Ambwene Yessyah a.k.a AY, pamoja na aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Faraja Kotta Nyalandu kama Mabalozi wao katika ‘Kampeni ya Tokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto.’

Mrembo Faraja Kotta na Msanii AY

Kufuatia uteuzi huu kwa upande wa Tanzania, AY na Faraja Kota wameahidi kusaidia ‘Kampeni ya Tokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto na wameonesha kuhamasishwa na heshima hii waliyopewa kutoa sauti zao kutetea ulinzi wa mtoto.
AY amesema kuwa amepewa heshima kubwa kwa kuteuliwa kuwa Balozi wa UNICEF Tanzania na kuahidi kujitoa katika kutumia sauti na umaarufu wake kusaidia kutokomeza ukatili dhidi ya watoto hapa Tanzania.

Previous Post Next Post