Video vixen wa ‘My Gal’ Vera Sidika akiri kuwa na urafiki wa karibu na Rapper Prezzo wa kenya

Ili kumfahamu vizuri Vera Sidika aka Vee Beiby, chukua muda wako mchache kutazama video iliyowahi kuleta utata na kufungiwa Kenya ya P-Unit ‘You guy’, pamoja na video mpya ya Jackson Makini aka Prezzo ‘My Gal’.


Yes, huyo ndiye video vixen ambaye umbo lake na uzuri vimekuwa vikimpa nafasi ya picha zake kuzunguka kwa wingi katika mitandao, of-course kama ilivyo kwa Masongange wa bongo.

Mara baada ya video mpya ya King wa bling bling Prezzo kutoka mwezi uliopita, kuna habari zilianza kusambaa mtandaoni kuwa kuna uwezekano wawili hao wakawa na uhusiano zaidi ya ule wa kazi waliyoifanya, yaani kwa lugha nyingine inasemekana huenda wana-date.


Kuongezea Petrol katika uvumi huo, kwa mujibu wa Pulse, Prezzo na Vera Ijumaa iliyopita walionekana pamoja katika club moja huko Nairobi wakiwa na ukaribu wa kiasi hata cha kushare kinywaji, na baadaye usiku huo wawili hao walionekana wakiondoka eneo hilo na kuelekea kiwanja kingine.



Baada ya Vera kuhojiwa kama kuna chochote kinachoendelea kati yao, alisema ni kweli kuna kinachoendelea nyuma ya camera, lakini ni urafiki tu.

“Nina wasiwasi habari hizi zitavuruga uhusiano tulionao,” alisema Vera, “lakini ni kweli Prezzo na mimi tumekuwa na kitu kinaendelea chini ya radar. Ni rafiki yangu.”

Mrembo huyo aliendelea kuhoji, “ Oh my God! How did you even know about this? Who even told you I spend at his place”.

“Ni kweli sisi ni marafiki wa karibu. Siwezi kusema tuna kitu chochote kinachoendelea kama mnavyosema, lakini hiki ni kitu ambacho kilikuwa hakifahamiki toka 2009…I knew if the public knew how close we are we would get f***d up,” Alisisitiza.

Bofya Hapa Kutazama video aliyofanya Vera Sidika aka Vee Beiby,

Source: Standard Digital
Previous Post Next Post