Unataka Kujua ni kwa nini Haujatajirika, Hizi hapa ni sababu 7 zinazokuhusu wewe

Mambo, na Habari za kwako? leo katika safu yetu ya life style tunakulletea mambo 7 amabayo kama ungeyafanya pengine ungekuwa umetajirika so nimeona ni vema nikashare na wewe mambo muhimu katika maisha yetu .


Kuna tabia fulani zinazokufanya usifikie malengo ambayo unayafikiriaga muda wote.Sikulaumu, sisi wote hua mara moja au nyingine tunaangukia katika mambo haya.Sasa ni wakati wa mabadiliko kwasababu hivi ndio vitu vinavyozuia mafanikio yako.

Unatumia muda mwingi Facebook
Najua si vibaya kucheki what friends are up to now and then lakini muda unaotumia kulike status na picha za watu  ambazo hazileti tofauti yoyote katika maisha yako unasababisha upoteaji wa muda mwingi .
Unafikiri unafanya kazi kwa bidii lakini si kweli
Ni kweli unatumia siku nzima ofisini lakini mapumziko ,kusumbuliwa na kupoteza kusudi la kazi unayofanya vinachangia sana kupoteza muda wako kwa kiasi usichoweza kutegemea.Ushawahi kufikiria biashara ya pembeni itakayokuletea kipato ? je , unafanya nini muda  wa kazi unapoisha? Je, unatumia muda wako wa jioni kukaa kwenye kochi ukiangalia TV  au laprop ukicheki movies/series ? Huo ndio muda ambao unatakiwa ufikirie business idea uliyonayo, kazi ya nje au kitu chako mwenyewe ambacho kwa siku za baadae kitakua ndio kazi yako ya kudumu.
Hauna Ufanisi
Kwahiyo unaweza kusema unafanya kazi kwa bidii na haupotezi muda wako katika kazi zako lakini nataka nikuambie na sipendi kusema hivi – unaweza kufanya vizuri zaidi. Bdio, unafanya kazi kwa bidii lakini kuna njia ya kufanya kazi hiyo izae matunda.unajua msemo unaosema” Siyo tu  ufanye kazi kwa bidii, bali  ufanye  kazi nadhifu.”
Unakata tamaa kirahisia
  labda mambo hayajaenda kama ulivyotarajia au watu hawadhamini mchango wako na hii kukufanya kukosa motisha na msukumo wa kufanya kazi. Hauwezi kufikiria malipo ya miaka ijayo kwa kazi unayoifanya leo kazi utazofanya kwa siku,wiki hata mwezi na kulipwa ni nzuri na ndio ambazo watu wengi hupendelea.lakini kwa kila mtu aliyefanikiwa anajua kwamba ili uweze kujenga kitu au biashara imara na endelevu  inabidi uwekeze katika muda sasa na matokeo yake hayatajionyesha kwa miaka.kama hauwezi kukubaliana na jambo hili basi utakua haufikirii kwa upeo zaidi mambo ya  baadae.
Hau-take Risks
Najua.Ni vizuri zaidi kutoamua kutofanya kitu ambacho kinaweza kukwama baadae. kuacha ku-take risks ni vizuri lakini hakuna malipo bila kufanya kitu cha hatari kidogo. najua kuna vitu vizuri vinaweza kutokea bila mtu ku-take risk lakini ni mara ngapi biashara inajegwa na kukua kwa kutegemea bahati halisi.Taking risks inabidi iwe moja ya job description yako na japokua ukifeli haujisikii vizuri lakini unajua kipi kitakufanya ujisikie vizuru? kufeli , kufeli , kufeli na ghafla kufaulu na kufanikiwa. na sasa hautajisikia vibaya kuhusu kufeli kwako sababu kupitia kufeli huko ndio kulikufunza njia ya kufaulu.
Hautumii Opportunities
sio tu kuchukua risks bali hata kuchukua opportunities zinazotokea linaweza likawa jambo gumu. opportunities zenyewe zinakuja kwa kujificha ukitofautisha na risks.maranyingi mafanikio huja kwa kukubali kuchukua opportunities zinazotisha. tafuta opportunities kwenye sehemu ulizotegemea na utashangaa vitu utakavyogundua.
Naamini unaweza kufanikiwa,inabidi tu kuangalia hivi vitu 7 nilivyovizungumzia.
Previous Post Next Post