Solange mauzo ya nyimbo zake yaongezeka kwa 233% baada ya ugomvi wake na Jay Z

Skendo iliyotishia kuchafua sifa ya familia ya The Carters na The Knowles imegeuka kuwa faida kwa mdogo wake Beyonce ambaye pia ni mwimbaji.

Beyonce akiwa na Nduguye Solange
Licha ya kuwa kipande cha video ya CCTV kinachomuonesha Solange Knowles akimshambulia shemeji yake Jay Z kwenye lift May 5 kwenye Met Gala kuipa mitandao lishe yenye ‘vitamin’ za kutosha kwaajili ya wasomaji wao, lakini pia imempa faida Solange mwenyewe kwa kusaidia kumuongezea mauzo ya kazi zake.
Imeripotiwa kuwa mauzo ya mtandaoni (digital track sales) ya nyimbo za Solange yalipanda hadi kufika nakala 2,000 katika wiki ya May 18 ambayo video ya ugomvi huo iliposambaa, kutoka mauzo ya nakala 600 kwa wiki moja ya nyuma, kwa mujibu wa Nielsen SoundScan.
Inaaminika kuwa mauzo hayo yalichangiwa na jinsi skendo hiyo ilivyoripotiwa na vyombo vingi vya habari na kumfanya Solange awe midomoni mwa watu kwa wiki nzima.
Previous Post Next Post