Producer Manecky afunguka 'Niliacha kufanya kazi na Diamond Platnumz kwa sababu ya kuvujisha Nyimbo zake

Producer wa AM Records, Manecky amesema alisimama kufanya kazi na Diamond kwakuwa alikuwa akimharibia kazi zake kwa kupenda kuvujisha nyimbo ambazo zilikuwa hazijakamilika.




“Ujue wasanii wana mchezo ukimaliza kazi yake, anaomba demo na kuiweka kwenye simu yake, sasa wana katabia ka kuachia chinichini (kwa kuwarushia rafiki zao kwa simu) ili kusikiliza wadau wanavyopokea,” Manecky amesema kwenye mahojiano na Global TV. “Ikipokelewa vizuri, anaitoa au akiona ina upungufu fulani anaifanyia mabadiliko haraka. Ndicho kilichotokea kwa Diamond.Mimi nisingeweza kuachia singo yake bila idhini yake. Kwanza ili iweje? Halafu singo yenyewe iliyoachiwa ilikuwa haina hata lebo yangu, sasa ingekuwa na faida gani na mimi? Sijambo la kweli.Kwa upande mwingine mpaka nikasitisha kufanya naye project (Diamond) baada ya kuona mimi nafanya biashara yangu,nimetumia muda mwingi nimeinvest kwa kiasi kikubwa katika ofisi yangu,kwahiyo nikaona bora nisimamishe kufanya naey kazi kwasababu ananiharibia biashara.”
Previous Post Next Post