EAC kuimarisha vita dhidi ya ugaidi

Jumuiya ya Afrika Mashari imesema itahakikisha inapambana na vita dhidi ya ugaidi katika nchi wananchama wa jumuiya hiyo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais uhuru Kenyata

Mwenyekiti wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Uhuru Kenyetta wa kenya amesema nchi wanachama wa jumuiya hiyo zitahakikisha vita dhidi ya ugaidi inaendelea kuimarishwa na kuhakikisha wananchi wake wanaishi kwa amani.

Mh Rais Uhuru Kenyata amesema hayo baada kumalizika kwa kikao cha ndani cha marais wa nchi za Jumuiya hiyo ambacho nchi ya Rwanda iliwakilishwa na waziri mkuu na Burundi iliwakilishwa na makamu wa kwanza wa Rais.

Kuhusu hatima ya sudani kusini kujiunga katika jumuiya hiyo rais kenyata amesema jitihada zinaendelea za kuhakikisha kuwa amani inapatikana kwanza katika nchi hizo na ameendelea kuwataka viongozi kutimiza makubaliano yao yaliyowekwa hapo awali yakiwemo ya kusimamisha mapigano.

Aidha wakuu hao wa nchi za Jumuiya ya Afika Mashariki pia walishuhudia kuapishwa kwa majaji watatu wa mahakama ya jumuiya sambamba na kuzinduliwa kwa mtandao wa kuwawezesha wananchi wa nchi hizo kufungua kesi mahali popote walipo bila kufika mahakamani.

Hatua hiyo imemgusa msajili wa mahakama hiyo Prf John Ruhangisa ambaye amesema kuwa itapunguza changamoto nyingi zilizokuwa zinawakabili
katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Dkt. Richard Sezbera amesema baada ya kukamilika kwa mkutano huo baada ya kupokea mapendekezo mbalimbali ya baraza la mawaziri hatua inayoifuata ni maandalizi ya katiba ya ya shirikisho.
Previous Post Next Post

Popular Items