Mume Wa Flora Mbasha Atuhumiwa Kumbaka Shemeji Yake, Flora Apost Picha Za Mumewe Siku Hiyo Hiyo

Mume wa muimbaji wa injili Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha ambaye pia ni muimbaji anatafutwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17.

Kwa mujibu wa Global Publishershers, mwanaume huyo anasakwa na jeshi la polisi baada ya shemeji yake kuripoti katika kituo cha polisi Jumatatu wiki hii majira ya mchana na kufungua mashitaka dhidi ya mwanaume huyo akidai kuwa alimmbaka kwa nyakati tofauti katika siku mbili (Ijumaa na Jumapili) ya wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar es Salaam.



Imeelezwa kuwa mlalamikaji alifanyiwa kitendo hicho Jumamosi sebuleni kwa Mbasha, na Jumapili ndani ya gari la mlalamikiwa na kwamba kutokana na maumivu makali aliyosababishiwa aliamua kuripoti katika kituo cha polisi na kufungua kesi yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada la Uchunguzi Na. TBT/IR/1865/2014.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa kulikuwa na ugomvi mkubwa kati ya Flora na mumewe hali iliyomsababiha Flora kuondoka nyumbani na kuishi hotelini na nafasi hiyo mumewe aliitumia kufanya tukio hilo.

Global Publishers imeeleza kuwa ilizungumza na mlalamikaji kwa njia ya simu na alithibisha kufanyiwa kitendo hicho na mume wa Flora na kueleza kuwa tayari wameshatoa taarifa polisi.

Jumapili (May 25) ambayo mlalamikaji anadai alibakwa ndani ya gari na Emmanuel, Flora Mbasha alipost kwenye ukurasa wake wa Facebook picha mbalimbali za matukio mbalimbali akiwa na mumewe, huku picha ya mwisho ikimuonesha mume wake huyo akiwa nje ya hospitali ya kanisa huko Haydom, Mbulu (Haydom Lutheran Hospital) na kuandika ‘Haydom’.

Hata hivyo, tangu kuwepo na tuhuma hizo mwimbaji huyo wa kike hajapost chochote kwenye Facebook.

Jeshi la polisi bado halijatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo.
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa