Hiki ndicho kiasi cha fedha alichotoa Diamond Platnumz kufanya video yake mpya uingereza!

Unaambiwa ukitaka kitu kizuri sharti ukubali kuingia gharama kama jinsi amabavyo anafanya The Bongoflava Super Star Naseeb a.k.a Diamond Platnumz, Baada ya  kuchomoa kiasi cha Dola 25,000 sawa na Tsh millioni 40 za kitanzania kwa director Clarence Peters wa Nigieria kwa ajili ya kufanya production ya video ya number one remix aliyomshirikisha Davido ambapo ilijumuisha gharama za kila kitu hadi models na dancers .
Sasa jamaa ameamua kuchomoa mpunga huohuo yaani Dola elfu 25 kwa director MoE Musa ambae anaishi na kufanya kazi zake nchini Uingereza kwa ajili ya video yake mpya aliyomshirikisha Iyanya kutoka nchini Nigeria


Gharama hizo za Dola elfu 25 ($25,000) hazitajumuisha gharama za kumsafirisha Iyanya kutoka Nigeria pamoja na malazi na kila kitu anapokua nchini Uingereza. Kwasasa Diamond Platnumz yupo nchini Ghana ambapo anategemea kufanya  kolabo nyingine na Davido itakayowahusisha pia Tiwa Savage wa Nigeria na Mafikizolo wa South Africa ikiwa ni kampeni ya kituo kimoja kikubwa cha TV barani Afrika.
Previous Post Next Post

Popular Items