Hii ndio Idadi ya Wanawake wanaoendesha Ndege, Treni, Malori na Mabasi Tanzania

Ni mara chache sana tunapata takwimu kama hizi kutoka kwenye ngazi ya juu ya serikali ya Tanzania ndio maana hii stori imekua kubwa baada ya kutolewa na Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe bungeni Dodoma May 24 2014.



Waziri Mwakyembe amesema pamoja na ugumu wa kazi ya udereva Tanzania kuna madereva Wanawake watatu wa mabasi makubwa na Wanawake wawili wa malori ya mizigo kwenda Lubumbashi Congo.

Vilevile kuna Wahandisi Wanawake 15 wa mitambo kuongozea ndege, kuna Wanawake 8 madereva wa Treni, marubani 8 Wanawake, waongoza ndege 16 Wanawake.

Taharifa zimetolewa na Wizara ya Uchukuzi


Previous Post Next Post